Serikali yatoa ufafanuzi waliokufa kwa kula nyama msibani

Serikali imesema vifo vya Watu wawili vilivyotokea kwa ulaji wa nyama kwenye kijiji cha Msaranga kilichoko Kata ya Kisale, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro May 04 mwaka huu havihusiani kabisa na ugonjwa wa kimeta.


Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mifugo Tanzania Dkt. Benezeth Lutege imewatoa Wananchi hofu na taharuki iliyojitokeza Wilayani Rombo, baada ya majibu ya uchunguzi wa kimaabara kuthibitisha kuwa vifo hivyo havihusiani kabisa na ugonjwa wa kimeta ambao hutokana na kula nyama ya ng’ombe aliyeathirika na ugonjwa huo.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Wizara inawasisitiza Wananchi wa Kijiji cha Msalanga, Kata ya Kisale Wilaya ya Rombo na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya ikiwa ni pamoja na kununua nyama zilizokaguliwa na Wataalamu wa Mifugo waliosajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) na kutoka kwenye mabucha na maduka ya nyama yaliyothibitishwa na Serikali kupitia Bodi ya Nyama Tanzania (TMB).

Taarifa hiyo imesema ni vizuri Wananchi wakajua dalili za ugonjwa wa kimeta ambazo ni pamoja na kifo cha ghafla kwa mnyama aliyeathirika za sehemu zote zilizo wazi hutoa damu ambayo haigandi, pia Watu ambao hugusana au kula nyama ya mnyama mwenye kimeta, huonesha dalili za homa, kupumua kwa shida, kichefuchefu, kutapika na malengelenge kwenye ngozi dalili ambazo hazikuonekana kwa wale Wagonjwa wawili waliofariki katika tukio


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo