Mchungaji Antoni Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kutokana na tukio la waumini kufa kwa kuambiwa na mchungaji wao wasile hadi wafe, hakuwahi kufikiri kama nchini humo kunaweza kuwa na waumini wa namna hiyo.
Mzee wa Upako ameyazungumza hayo leo Mei 8, 2023 alipokuwa akifanyiwa mahojiano na East Aafrica Radio ambapo alieleza masuala mbalimbali.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mzee wa Upako anasema alikuwa akiamini Wakenya wengi wana akili lakini tukio hilo limemshangaza.
"Sikuwahi kuwaza kama Kenya kunaweza kuwa na mabwege kama wale, nilikuwa najua Kenya inaongoza kwa wasomi lakini kwa hili tukio wamenishangaza," alisema Mzee wa Upako.
