Kumbi za starehe 89 zafungwa kwa kelele, DAR yaongoza

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Samuel Gwamaka amesema jumla ya baa na kumbi za starehe 89 zimefungiwa baada ya kubaini kupiga kelele na mitetemo iliyozidi viwango vinavyotakiwa.


Dk Gwamaka amesema baa na kumbi hizo za starehe zimebainika katika operesheni iliyofanyika ndani ya wiki moja katika majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Ameeleza hayo leo Jumatatu, Mei 8, 2023 wakati akitoa mrejesho wa msako walioufanya kati ya NEMC na jeshi la polisi kubaini baa na kumbi za starehe zinazopiga muziki kwa sauti ya juu ambayo ni kinyume cha sheria ya mazingira ya mwaka 2014.

"Tumebaini na kufunga baa na kumbi za starehe 19 za Kinondoni, 25 Ilala, Kigamboni 22 na Temeke 12, jijini Dodoma ni tano na Mwanza ni sita. Maeneo haya tulioyafunga ni sugu na haikuwa mara kwanza kuwaonya hawa tuliowafungia,” amesema


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo