Diwani alia na Ubovu wa barabara "Wananchi wanachanga fedha zao"

Diwani wa kata ya ya Ikuwo wilayani Makete mkoani Njombe amesema kwa sasa wananchi wanalazimika kutumia gharama zao (kujichanga) ili kuifanyia matengenezo barabara ya Ikuwo - Nkenja ili ipitike kwa gari kwa kuwa imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha


Akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Mei 4,2023 Diwani huyo amesema kwa sasa barabara hiyo haipitiki kwa gari, hivyo kuiomba TARURA kuiangalia kwa ukaribu barabara hiyo ambayo inahitaji matengenezo

Diwani Mwasanga Amesema barabara hiyo ina umuhimu kwa kuwa wananchi huitumia kwa kusafirisha mazao na wao wenyewe wakiwemo wagonjwa wanaofuata huduma za kiafya katika hospitali ya wilaya ya Makete.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo