MWANAMKE aitwaye Jackline Mnkonyi mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa Sombetini jijini Arusha amekutana na kipigo kutoka kwa mume wake, Isaac Mnyagi na kung’olewa meno mawili pamoja na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambua na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini.
Alisema raia waliomfahamu ndio walimtambua na kuwapigia simu wazazi wake na walipofungua geti waliamua kumchukua na asubuhi alipelekwa hospital kwa matibabu.