Afuta Harusi Yao Baada ya Mchumba Wake Kumpa 'EX' Wake Kadi ya Mwaliko

Mwanamke raia wa Nigeria amejawa na machozi baada ya mchumba wake kufuta harusi yao.


Mrembo huyo alianika suala hilo kwenye kundi la Facebook na kuomba ushauri wa wanamtandao Alisema alimtembelea tu mpenzi wake wa zamani ili kumpa kadi ya mwaliko kwenye harusi yake, lakini aliishia kurusha roho na jamaa huyo. 


Kwa bahati mbaya, mume wake mtarajiwa aligundua kuhusu uzinzi wake baada ya kudukua simu yake.


Baadaye mwanamume huyo aliagiza kwamba matayarisho yote ya harusi yasitishwe mara moja.


Mrembo huyo alilalama kuwa: "Mbele yangu, aliwaita wazazi wote wawili na kuwataka wasitishe maandalizi yote ya harusi. Walipouliza kwanini, aliwaambia nitaeleza vizuri zaidi. Aliniacha nyumbani kwake na kwenda hotelini na hakurudi"


Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo