Wanawake walia kutelekezewa watoto waliozaa na Wachina

Kwa zaidi ya muongo uliopita, Wachina wamekuwa wakifurika mijini na vijijini barani Afrika kujenga barabara, mabwawa, madaraja na miundombinu mingine ya kisasa


Hata hivyo, kuja kwao kumeleta baraka na masaibu kutokana na kuhusika katika mauhusiano ya kimapenzi na wenyeji na matokeo kuwa watoto wa rangi tofauti. Lakini tatizo ni kwamba wanawake waliozaa watoto na Wachina hao hujipata kwenye njia panda baada ya mradi huo wa ujenzi kumalizika na raia hao wa kigeni kuondoka.


Watoto waliozaliwa kutokana na mahusiano hayo pia wana ugumu wa kutangamana na wenzao kwa sababu wanaonekana tofauti sana na wakati mwingine husababisha wao kudhihakiwa.


Atelekezwa na watoto Katika taarifa ya awali, TUKO.co.ke iliripoti kuhusu kisa makahaba waliolalamikia kuachwa na Wachina hao baada ya kuwazalia watoto. Kwa mfano mjini Karuma kando ya Barabara Kuu ya Kampala-Gulu, kulikuwa namradi wa ujenzi wa mtambo wa Karuma Hydro Power wa megawati 600 kando ya Mto Nile. 


Mwanawake mmoja ambaye aliomba jina lake kubanwa alifichua kwamba alikuwa akiendelea na biashara zake wakati mwanamume Mchina alipoonyesha kupendezwa naye. "Alianza kunifuata kupitia kwa polisi wa kike ambaye alimwambia ananipenda na alitaka kunioa," alisema. Muda si muda, Mchina huyo alimuahidi kazi katika eneo la ujenzi, ahadi ambayo ilitimizwa wakati nafasi za wapishi zilipopatikana.


Mambo yalipokuwa yakiendelea kusonga mbele, Mchina huyo alimbaka na matokeo yake kusababisha kuzaliwa kwa mtoto wa rangi tofauti, a kisha mwanamume huyo alitoweka. Juhudi zake mwanamke huyo kutafuta haki ya kumshurutisha mwanamume huyo achangie katika malezi ya mtoto mwanao, hayakufua dafu kwani mamlaka hazikufanya za mno kumsaidia. Inafahamika kuwa bajeti nyingi za miradi ya Wachina zina mgao mbalimbali unaokusudiwa kwa shughuli za CSR ndani ya jamii. Hiyo ni kinyume na mradi huo kuwa na bajeti ambayo ilitengwa kutunza watoto walioachwa na wakandarasi. 


Mwenyekiti wa baraza la mji wa Karuma Washington Ochaya alifichua kuwa kufikia sasa anafahamu zaidi ya visa 14 vya watoto chotara katika eneo lake, tatizo ambalo analazimika kukumbana nalo kila siku. Pamela Angwech ambaye anaendesha shirika lisilo la kiserikali la kusaidia wanawake katika eneo hilo, aliongeza kuwa kupata haki ni vigumu kwani wahalifu wengi huhamishwa pindi kesi inapowasilishwa kwa kampuni yao.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo