Familia Yatupa Jeneza la Mazishi ya Mama yao, Kisa limenunuliwa na Mkwe

 

Siku ya Alhamisi, Mei 30,2023 familia moja ilitupa jeneza ambalo mkwe alinunua kwa ajili ya mazishi ya mama mkwe wake.


Mtumiaji wa Facebook, Bem Raphael Aondongu, ambaye alishiriki hadithi hiyo, alisema tukio hilo lilifanyika Tombo Mbatie, katika eneo la Buruku katika jimbo la Benue. 


Bem alisema wana wa marehemu walikataa jeneza hilo kwani familia iliona si zuri na la bei rahisi kutumiwa kwa marehemu mama yao. Akielezea kuhusu mila ya TIV iliyomlazimu mkwe kupeana jeneza, Bem aliandika:


“Kama mila ya TIV inavyodai, mama au baba anapofariki, mtoto wa kwanza wa kike ambaye ameolewa ndiye anayebebeshwa jukumu la kuandaa jeneza kwa ajili ya mazishi ya mzazi yeyote kati ya waliofariki. “Na kwa ajili ya kudumisha mila, mtoto wa kwanza wa kike kwa kushirikiana na mumewe ambaye ni mkwe wa marehemu mama, walijaribu kadri ya uwezo wao kuleta jeneza hili kwenye picha hapa chini lakini lilikataliwa. "Kwa mujibu wa familia ya marehemu, walisema jeneza hilo halikuonekana vizuri na lilionekana kuwa la mtu maskini sana..."


Chanzo: TUKO.co.ke


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo