Mahakama Kuu ya Tanzania imempa siku 14 za kazi mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wenzake watatu kumlipa Waziri wa Mambo ya Nje Mstaafu, Benard Membe TZS bilioni 9.92 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vya habari.
Mahakama imetahadharisha deni hilo lilipwe ndani ya muda vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.
Hukumu ya shauri la kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, ilitolewa tarehe 28 Oktoba, 2021 na Jaji Joacquine De Mello, ambapo Musiba anatakiwa kulipa fedha hizo lakini pia kulipa gharama za kesi hiyo.
Katika kiasi hicho cha fedha, Shilingi bilioni tano ni fidia ya hasara halisi na Shilingi bilioni moja hasara ya jumla.
Alisema hukumu hiyo pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.