Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, linamshikilia Askari wa Jeshi hilo, namba H.4489 PC Kaluletela wa Kituo cha Polisi Sirari, baada ya askari huyo kumfyatulia risasi mwananchi aitwaye Ng'ondi Marwa Masiaga (22), mkazi wa Mtaa wa Regoryo wilayani Tarime, mfanyabiashara wa bodaboda na kusababisha kifo chake.
Katika Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, imesema askari huyo kwa uzembe wake mwenyewe, alimfyatulia risasi raia huyo asiyekuwa na hatia na kumjeruhi kwenye paja lake la mguu wa kulia.