Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Mrakibu wa Polisi Mossi Ndozero amewakamata madereva wa mabasi Kampuni ya Saul, Superfeo pamoja na Newforce kwa makosa mbali mbali ikiwemo mwendo kasi.
Katika mtego wake ulioambatana na oparesheni maalumu kwa watuamiaji wa vyombo vya moto Ndozero aliweka mtego kwa madereva wa mabasi hayo kutokana na kupokea taarifa za awali kuwa mabasi hayo yalikuwa yanakimbizana bila kujali usalama wa abiria waliowabeba
Amewataka madereva hao kuripoti ofisini kwake wakiwa na leseni zao na kwamba kwa yeyote atakayekiuka maagizo hayo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo dereva wa basi la Superfeo aliingia mitini baada ya kugundua amefanya makosa na kutokomea kusikojulikana na kumlazimu dereva wa pili kuchukua jukumu la kuendelea na safari kuwasafirisha abiria waliokuwemo kwenye basi hilo.