Polisi Wawaokoa Watu 100 Waliofungiwa Katika Kanisa la Mchungaji Ezekiel

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amethibitisha kuwa polisi walivamia Kituo cha Maombi na Kanisa la New Life Alhamisi, Aprili 27, 2023 na kuwaondoa waumini walioishi hapo.


Kulingana na Kindiki, watu karibu 100 walioishi kwenye majengo ya kanisa wwalifunguliwa lakini walipelekwa katika kituo cha polisi karibu na hapo ili kurekodi taarifa.


Wakati uo huo, kiongozi mkuu wa kanisa, Pasta Ezekiel Odero, yupo kizuizini mwa polisi baada ya kukamatwa Alhamisi, Aprili 27. Anatazamiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayohusiana na mauaji ya halaiki ya watu.


"Inatangazwa kwa taarifa ya umma kwamba Bwana Ezekiel Ombok Odero, kiongozi wa Kituo cha Maombi/Kanisa cha New Life huko Mavueni ndani ya Eneo la Kilifi Kaskazini katika Kaunti ya Kilifi, amekamatwa na anapitia kipindi cha kushughulikia mashtaka ya jinai yanayohusiana na mauaji ya wafuasi wake. 


Kanisa hilo limefungwa. Watu zaidi ya 100 ambao walikuwa wamefungiwa hapo wameondolewa na watatakiwa kurekodi taarifa," Kindiki alisema katika taarifa.


Mamlaka katika Kaunti ya Kilifi pia ilifichua sababu za kukamatwa kwa mhubiri huyo maarufu. Sababu ya kukamatwa kwa Ezekiel ulifichuliwa na Kamishna wa Kikanda wa Pwani Rhoda Onyancha. 


Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kutiwa nguvuni, Onyancha alithibitisha kuwa polisi wanamzuilia mhubiri huyo kuhusu vifo vilivyotokea katika kanisa lake. "Tumemkamata kwa madai ya vifo vinavyotokea katika majengo yake na kuripotiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mbalimbali," alifichua.


Msimamizi huyo pia alitangaza majengo ya kanisa yamefungwa hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo na kuwaambia wananchi kuepukana na eneo hilo.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo