Mlinzi wa Msikiti auawa Kinyama

 

Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi Bakari Kasarani (46) ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana katika msikiti wa Shree Hindu Mandal Temple Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.


Akisimulia kuhusu tukio hilo, Msimamizi wa msikiti huo Niraj Kakad amesema mlinzi huyo alikutwa ameuawa nyuma ya msikiti na vitu ambavyo bado thamani yake haijajulikana vimevunjwa ikiwemo sanamu inayoabudiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amelaani tukio hilo la kikatili na kuagiza Jeshi la polisi kufanya uchuguzi wa tukio hilo ili watu waliofanya unyama huo watafutwe mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo