Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi imelaani na kukemea vikali vitendo vya mabinti kuvaa mavazi yasiyokuwa na maadili na kuwataka wazazi kuangalia namna ya kulikomesha hili ili kujenga kizazi kitakacho kuwa na maadili mema
Akizungmza mara baada ya kumaliza ziara kwenye Kata tatu za jimbo la Mafinga Mjini Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Festo Kilipamwambu amesema katika ziara hiyo wamejinea changamoto mbali mbali huku mmomonyoko wa maadili kwa watoto ukiwa ni changamoto kubwa inayoikabili jamii kwa sasa
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mufindi Josina Kinyamagoha amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa viongozi wa jumuiya walioko kwenye kata ili wao wakatoe elimu kwa jamii inayowazunguka ili kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili unayoikumba jamii kwa sasa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Mufindi kupitia Jumuiya ya Wazazi Dkt.Bazil Tweve amesema pamoja na elimu ya uongozi inayoendelea kutolewa kwa viongozi wa jumuiya lakini pia elimu ya uchumi imeendelea kutolewa ili kuondokana na hali ya viongozi au jumuiya kuwa tegemezi
Katibu Elimu,malezi na mazingira wa jumuiya ya Wazazi Wilaya Wilaya ya Mufindi John Mgina ameeleza changamoto ya baadhi ya wanafunzi wa kike kuwa wanajiuza huku baadhi ya wazazi wakilia na serikali kuona njia mbadala ya kukomesha jambo hilo
Ziara hii imefanyika katika Kata ya Isalavanu,Rungemba na Kata ya Kinyanambo.