Marekani kupitia Makamu wake wa Rais Kamala Harris imesema katika mradi wa uwekezaji dhidi ya Malaria kupitia Mpango Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Malaria (PMI): imepanga kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 39 sawa na Shilingi bilioni 89.7 za Tanzania katika kipindi cha mwaka mmoja ujao katika ubia na Serikali ya Tanzania katika kuendesha miradi ya kupambana na malaria iliyothibitika kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na vyandarua, dawa dhidi ya malaria zinazofanya kazi kwa haraka, vifaa vya upimaji wa haraka, na matibabu kinga kwa akina mama wajawazito.
Fedha hizi zinakusudiwa kusaidia mfumo ulioimarishwa zaidi wa afya kupitia mafunzo kwa wahudumu wa afya, kuimarisha mnyororo wa ugavi na kuboresha ufuatiliaji wa data.