Kulikuwa na mshtuko baada ya mrembo kumeza pete ya uchumba ambayo mpenzi wake alikusudia kuitumia kumposa.
Jessicah Hawayu kutoka katika kaunti ya Tana River nchini Kenya, alikuwa amejumuika pamoja na familia yake kwa nyumbani kwake Ganjoni kwa karamu bila kujulishwa ilikuwa ni siku yake ya kuposwa.
Katika mpango huo, mama yake Hawayu ndiye alikuwa na jukumu la kuiweka pete hiyo kwenye sahani yake ya pilau.
Lakini nusra raha ya uchumba igeuke karaha wakati Hawayu alionekana kusakamwa na chakula kooni.
Baba yake alimuinamisha na kumpiga konde mara tatu hadi pete ikaruka kutoka kooni.
Chanzo: TUKO.co.ke