Mshtakiwa aomba ugali kizimbani ili apate nguvu kujibu mashtaka


Japhet Olindo ambaye ni mwanajeshi wa Kenya alichekesha umma uliofika mahakamani Eldoret jana Jumatatu, alipomlilia hakimu akimuomba apewe ugali ale ili apate nguvu ya kujibu mashtaka, tovuti ya Taifa Leo imeripoti kisa hicho.


“Mheshimiwa, kabla sijasomewa mashtaka naomba uninunulie ugali, nina njaa sana sijapewa chakula tangu niwekwe selo, ninakaribia kuzimia tafadhali fanya jambo kabla sijaanza kushtakiwa,” alisema Olindo. Ilibidi hakimu Keynes Odhiambo aweze kumbembeleza na kuahidi kumnunulia ugali, ndipo akakubali kujibu shtaka lake la kumjeruhi mtu

Nimesikia kilio chako kwa leo nitakununulia ugali kabla hujaondoka hapa kortini jibu shtaka kwanza na mimi nitatimiza ahadi yangu,” alimuahidi Odhiambo. Vilevile Olindo alimwambia hakimu huyo mwandamizi mkuu kuwa anahofia endapo akipewa dhamana asiyoweza kuimudu, huenda mkewe akachukuliwa na wanaume wengine akiwa mahabusu (korokoroni).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo