Serikali ya Marekani kupitia Makamu wake wa Rais Kamala Harris ambaye yupo ziarani Tanzania imeahidi kutoa Huduma za Ushauri wa kitaalamu kuhusu Uendeshaji na Biashara ya Bandari (Port Transaction Advisory Services):
Programu hiyo inalenga kusaidia jitihada za Serikali ya Tanzania kutumia kikamilifu fursa za uwekezaji na kuvutia wawekezaji wa aina mbalimbali, kulinda uwekezaji wake wa kifedha na kuimarisha udhibiti wake, kama nchi huru, wa miundombinu hii muhimu.