Marekani kutoa Bilioni 995 Mapambano dhidi ya UKIMWI Tanzania

Serikali ya Marekani imesema kuwa itaendelea na katika Mpango wa Dharura wa Rais wa nchi hiyo wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania, ambapo Marekani inapanga kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 433 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 995 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi 12 zinazoshiriki katika Muungano wa Kimataifa Kutokomeza UKIMWI kwa Watoto, muungano unaoongozwa na Shirika ya UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) na Ofisi ya Mratibu wa Shughuli za Kupambana na UKIMWI Kimataifa.

Kwa ubia na Serikali ya Tanzania, PEPFAR inasaidia kuandaliwa kwa sera za afya zitakazoimarisha programu na afua za VVU kwa watoto. 

PEPFAR inaisaidia Tanzania kuweka sera za afya zitakazoimarisha afua dhidi ya VVU zinazowalenga Watoto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo