Kitimoto yapigwa Marufuku, Faini Milioni 1.2


Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imepiga marufuku uingizwaji wa Nguruwe na matumizi ya mazao yatokanayo na nguruwe wilayani humo.

Akizungumza na vyombo vya habari jana Machi 15, 2023 Daktari wa mifugo wilayani humo Festo Mkomba amesema zuio hilo limekuja baada ya  kubainika kwa uwepo wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe.

Ameongeza  kuwa zuio litadumu mpaka pale itakapotolewa ruhusa kwa wananchi kuanza upya matumizi ya mnyama huyo.

“Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya mifugo namba 16(2),17 ya mwaka 2003 kuanzia leo 15/03/2023 mimi Dkt. Festo Mkomba (BVM) Daktari wa mifugo Wilaya ya Ludewa natangaza kwamba Ludewa itakuwa chini ya karantini mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo, hii ni kutokana na matukio ya ugonjwa wa homa ya nguruwe kujitokeza katika Wilaya ya Ludewa, Amesema Mkomba.

Ameongeza kuwa kwa yeyote atakaye bainika kuendeleza huduma hizi atachukuliwa hatua kali za sheria ambapo moja ya sheria hizo ni kifungo cha miezi sita jela, faini ya sh. Milioni 1,200,000 ama vyote kwa pamoja.

Pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuutokomeza ugonjwa kwa haraka

“Naomba tutoe ushirikiano kwenye kuhakikisha hakuna mtu anavunja mashariti yaliyowekwa, kwani tukifanya hivyo huu ugonjwa huwa unaisha haraka sana (unapita) na baada ya hapo tunaendelea na utaratibu wetu wa kuchinja au kula kitimoto kama kawaida.” Amesema Mkomba


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo