Jafari Hamis Chabakari mwenye umri wa miaka 16, Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Mnima Mkoani Mtwara amekutwa amejinyonga porini kwa kutumia kamba.
Kaimu RPC Mtwara, Isack Mushi amesema tukio hilo limetokea February 26,2023 katika Kijiji na kata ya Mnima Wilaya na Mkoa wa Mtwara.
“Siku ya tukio Jafari alitoka nyumbani kwao na haikujulikana alipokuwa ameenda na ndipo baadaye mwili wake ulikutwa ukiwa porini, Mashahidi wameeleza kuukuta mwili ukiwa unaning'inia juu ya mti na kamba shingoni.
“Baada ya uchunguzi wa kitabibu kufanyika, Daktari alibaini kuwa chanzo cha kifo hicho ni kukosa hewa baada ya kubanwa na kamba shingoni, pia uchunguzi wa awali umebaini kuwa Marehemu alikuwa anatuhumiwa kuiba fedha Tsh 8,000 ambapo hata hivyo Mama yake alilipa fedha hiyo kuepusha usumbufu”
“Uchunguzi zaidi wa tukio hili unaendelea ili kujua sababu hasa ya kujinyonga”