Wizi wa alama za barabarani Tishio, Mkuu wa mkoa atoa Maagizo

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda, amewaagiza wakuu wa wilaya na jeshi la polisi kuwakamata watu wanaoharibu miundombinu ya barabara kutokana na kukithiri kwa wizi wa alama za barabarani na watu kwenda kuuza vyuma chakavu.


Dkt. Nawanda amesema serikali inatumia fedha nyingi kutengeneza miundombinu ya barabara lakini wapo watu wanaihujumu kwa kuiba alama za barabarani na kuisababishia hasara serikali huku akiliagiza jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kufanya ukaguzi wa kushitukiza maeneo yote wanapouza vyuma chakavu ili kubaini iwapo kama kuna alama za barabarani zinauzwa kama vyuma chakavu.

"Hii ni changamoto kubwa kwenye Mkoa huu sasa tuna kazi kubwa ya kufanya ili kukomesha wizi huu ambao unaisababishia serikali hasara kubwa,jeshi la polisi lifanye kazi yake,wakuu wa Wilaya,Tarura na Tanroads mhakikishe mnafanyakazi kama nilivyoelekeza kamateni wote watakaobainika wanahujumu miundombinu yetu"alisema Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Nawanda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara Mkoa wa Shinyanga (Tanroads) Mibara Ndirimbi amesema mpaka sasa alama za barabarani 50 zimeibiwa huku gharama ya kutengeneza alama moja hadi kukamilika na kuwekwa barabarani ni Shilingi laki tano na tatizo hilo limekuwa ni changamoto hasa maeneo ya mijini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo