Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe mkoani Songwe wakiongozwa na Mhe. Philipo Mulugo, Mbunge wa Jimbo la Songwe wamempigia magoti Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakimuomba ujenzi wa barabara kiwango cha lami kutoka Mbalizi - Mkwajuni - Patamela hadi Makongorosi.
Madiwani wameomba barabara ya lami wakati wa ziara ya siku moja aliyoifanya Waziri Mkuu Wilayani Songwe Februari 13, 2023.