Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, ameagiza kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa Dereva ambaye ameonekana katika kipande cha video akiendesha gari aina ya Nissan huku mbele kukiwa na Askari wa Usalama Barabarani akijaribu kumsimamisha
Amesema;
“Naagiza apelekwe kwenye Vyombo vya Dola na Leseni tuliyompa anyang’anywe kabisa. Haiwezekani Askari yupo Kazini anakuzuia wewe unampelekea Gari, nina wasiwasi na Akili za Madereva wetu sasa hivi, huyo lazima atakuwa na shida mahali.”