Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji, amesema serikali imetoa vibali kwa baadhi ya wafanyabiashara nchini kuingiza mchele tani elfu tisini, ambazo zinatarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu.
Waziri Kijaji amesisitiza kuwa, serikali haitarajii ongezeko la bei ya bidhaa zinazotumika kwa wingi katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kwaresma, ikiwemo sukari na unga wa ngano.
Waziri Kijaji ametoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa juu ya mwenendo wa bei za bidhaa muhimu nchini kwa mwezi wa pili.