Shirika la ndege la Precision Air, limesema rubani aliyekuwa akiendesha ndege ya shirika hilo, yenye namba PW 600, kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma, alilazimika kuzima injini mojawapo ya ndege hiyo na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), baada ya kupokea taarifa ya uwepo wa hitilafu kwenye moja ya injini ya ndege hiyo.
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bw.Hilary Mremi ,ambapo amebainisha taratibu za kutafuta ndege nyingine ili kuwasafirisha abiria hao zimefanyika.