Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linawashikilia Joyce Julius na Juma Charles (wanandoa), kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wao Butamo Igionzela (70) ambaye ni mama mzazi wa Joyce mkazi wa Bungezi kata ya Ihanamilo wilayani Geita wakimtuhumu kumuua mtoto wao kwa njia ya kishirikina
Akiongea na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Berthaneema Mlay amesema watuhumiwa hao wamefanya tukio hilo baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji kuwa mama yao alimuua mtoto wao
Aidha Mlay ameitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa kwenye vituo vya Polisi ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria