Tundu Lissu afungukia kauli ya 'kuunga mkono ushoga'


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania Bara, Tundu Antipasi Lissu amesema hajawahi kutaja popote kuwa anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja (ushoga) ila ni kampeni chafu zilizoundwa na baadhi ya mahasimu wake ili kumchafua.


Lissu amesema hayo wakati akijibu swali kwenye mahojiano maalum aliyofanya na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania ikiwa ni wiki moja tangu arejee kutoka nchini Ubelgiji alikokuwa akiishi kama mkimbizi wa kisiasa.

“Zile ni siasa za maji taka tena yale ya mtaroni, mimi sijawahi kusema kokote kule Duniani kwamba nina unga mkono mapenzi ya jinsia moja, sijawahi kusema.

“Nafahamu yalikotokea, nilifanya mahojiano na Hard Talk ya BBC, yule bwana akanibana sana kuhusu hili, majibu yangu yalikuwa ni kwamba, Serikali haitakiwi kuingilia mambo ya mambo ya farahga.

“Tulisharuhusu Serikali (kwa maana ya polisi na usalama) waje vyumbani mwenu kutazama mnachokifanya mkijifungia, itakuwa nchi ya namna gani ambayo huwezi kukaa na mwenza wako mkapata faragha?

“Nchi hii ina katiba inayosema, Serikali hairuhusiwi chumbani. Kila mtu ana haki ya kulindwa faragha yake (right to privacy) Tukiiruhusu Serikali ikaingia chumbani tumekwisha, hiki ndicho nilichosema… sasa ikaanzia hapo kuwa huyu anaunga mkono ushoga.

“Watu wenye Utamaduni huo wa Ushoga waendelee utamaduni wao, sisi wenye utamaduni tofauti, tuendelee na utamaduni wetu. Sheria zetu na utamaduni wetu hauruhusu ushoga, tuendelee na utamaduni wetu. Naunga mkono katiba yatu, mimi siungi mkono ushoga, ningekuwa naunga mkono ningesema,” amesema Tundu Lissu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo