Sheikh Alhad aliyetumbuliwa atoa kauli

Baada ya Sheikh Alhad Mussa Salim kutenguliwa nafasi ya kuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kiongopzi huyo wa dini ya Kiislam amesema ataendelea kuwa ndani ya Baraza katika nafasi nyingine.


Akizungumza na Clouds FM amesema; “Sijapewa taarifa rasmi lakini sina sababu ya kukata rufaa. Ni maamuzi ya Baraza, ni chombo chetu tumekiweka na kina Mamlaka ya kufanya hivyo. Kwanini wameniondoa sijui, nadhani watayataja wao.”

Baraza la Ulamaa katika kikao chake kilichoketi jana jijini Dar, kilitengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum, kama Sheikh wa mkoa wa Dar kuanzia Februari 2, 2023.

Baraza hilo lilimteua Sheikh Walid Alhad Omary kuwa Kaimu Sheikh wa mkoa wa Dar kuziba nafasi ya Sheikh Alhad.

Itakumbukwa wiki jana Sheikh Alhad kwa kushirikiana na baraza la masheikh wa mkoa wa Dar, alivunja ndoa ya Juma Mwaka na mkewe Queen, lakini kesho yake Baraza la Ulamaa lilibatilisha uamuzi huo na kufuta talaka hiyo.

Hata hivyo Sheikh Alhad aliemdelea kusisitiza kuwa talaka hiyo ni halali na ndoa hiyo imevunjwa.

Kesho yake Baraza la habari la habari la BAKWATA lilitoa tamko la kupinga maamuzi ya Baraza la Ulamaa na kusema linasimama na Sheikh Alhad kuvunja mdoa hiyo.

Baraza la Ulamaa ambalo ndio chombo kikuu cha maamuzi ndani ya BAKWATA lilitoa onyo kwa Masheikh hao pamoja na Sheikh Alhad, na kuwataka waombe radhi.

Hata hivyo hawakuomba radhi, mpaka jana Sheikh huyo alipopigwa na kitu kizito.!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo