Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, amesema kwamba kiuhalisia hakuna ajali ya ndege ya abiria iliyotokea wilayani humo na kwamba kilichofanyika leo ni zoezi la utayari wa kukabiliana na ajali za aina hiyo lililoandaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Mhita amesema zoezi hilo hufanyika kila baada ya miaka miwili na hakuna vifo vilivyojitokeza.
“Tulipokea taarifa ya ajali ya ndege tukafika eneo la tukio tukaja kutambua ni zoezi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kujipima utayari wa kuokoa, walifanya hilo zoezi kwa usiri mkubwa sana kwasababu wote tulifika hapa, navishukuru Vyombo vyote ambavyo vipo Kahama kwa utayari hata kama walikuwa kwenye utayari imenisaidia kujua Vyombo vyetu vipo na utayari, nimefika eneo la tukio nikaambiwa ni zoezi la kujipima”.