Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Bi Janeth Mayanja amesitisha shuguli na mafunzo kwa wajasiliamali yaliyokua yanatolewa na Kampuni ya Alliance In Motion Global ambayo inafanya biashara za mtandao.
Awali kampuni hiyo iliahidi kutoa mafunzo bure lakini imebainika mafunzo hayo kiingilio ni Tsh 20,000/= na baada ya mafunzo unalipia Tsh 600,000/= na unapewa bidhaaa za tiba lishe kwa ajili ya kuuza na jukumu la kuunga watu wengine na wao hulazimika kulipia 600,000/= na muingizaji hupata 'commission'.
Hivyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang amesitisha mafunzo hayo na kuwataka wakufunzi kuondoka katika Wilaya hiyo hadi pale uongozi wa Wilaya utakapojiridhisha na usahihi na shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo kutoka mamlaka mbalimbali zinazohusika.
Amewaomba Wananchi wa Hanang kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo Wilayani Hanang na kuacha kujiunga na Kampuni ambazo utaratibu wake wa uendeshaji haueleweki kuepusha kutapeliwa fedha.