Mtume Mwamposa aweka wazi suala la kuitwa Freemason

 
Kiongozi wa Kanisa la Arise and Shine (Inuka Uangaze) lililopo Kawe jijini Dar es Salaam, Mtume na Nabii Boniface Mwamposa amesema anawashangaa watu wanaomuita yeye ni freemason kutokana na staili yake ya maisha.


Mwamposa ambaye amekuwa maarufu katika huduma yake ya uchungaji hasa kwa kutumia mafuta ya upako, amesema hayo  Jumapili, Februari 12, 2023 wakati akizungumza na waumini wake kanisani kwake.

Aidha, Mwamposa amedai baadhi ya watu wamekuwa wakihoji maamuzi yake ya kubadili Viatu anapokuwa Kanisani akidai anafanya hivyo kwa kuwa kuna Viatu ambavyo vikimwagikiwa na Mafuta vinaharibika.

"Kila kitu nikifanya inakuwa gumzo, juzi nilikuwa Bungeni, nilifanya ibada kwa Wabunge, nilipotoka pale nashangaa picha zinazagaa kuhusu mimi kwa mabaya licha ya kuwa watumishi tulikuwa wengi.

Mwamposa amesema: "Yaani mimi nianze kujibizana na watu kwenye mitandao wanavyosema Mwamposa Freemason, nami niingine kwenye mitandao kuanza kuwajibu kuwa mimi si Freemason, sina muda huo hata kidogo.

"Hata nikiwa hapa (Kanisani) huwa wanashangaa ninavyobadilisha viatu, nabadilisha kwa kuwa mafuta ninayotembea nayo yakimwagikia kwenye kiatu yanakiharibu, hivyo nafaa viatu ambavyo nakuwa comfortable kuzunguka nacho.

"Hata wakiona nimevaa cheni inakuwa gumzo, hata nikichukua kitambaa hapa madhabahuni nikafuta jasho naambiwa Mimi ni Freemasons kwanini?" Amehoji Mtume Wenu Mwamposa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo