Mwanaume mmoja kutoka nchini Nigeria, amelitaka kanisa lake kumrudishia pesa zote alizotoa kama fungu la kumi kwa miaka mingi akidai hana hamu tena ya kuingia mbinguni.
Kufuatia video yake mitandaoni mwanaume huyo ambaye alikuwa akiabudu kwenye kanisa la Dunamis International Gospel Centre, lililopo nchini humo, amesema kuwa kwa miaka mingi, mchungaji wake amekuwa akitumia kitabu cha Mathayo 6:19 kumshawishi kuwekeza katika ufalme wa Mungu.