Fei Toto apata ajali ya Gari Zanzibar


Mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania Feisal Salum Abdallah (Fei toto) amepata ajali mchana wa leo Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.


Ajali hiyo imehusisha Gari yake aina ya Harrier nyeupe yenye namba za usajili Z 160 MW huku dereva akiwa ni mwenyewe Feitoto akitokea Fuoni kituo cha zamani akielekea Mjini ndipo ilipogongana na Bodaboda yenye namba za usajili Z 423 KL.

Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha wala kuumia zaidi ya Gari kuharibika mbele na Bodaboda imeharibika ambapo mpaka sasa Vyombo hivyo vipo kituo cha Polisi Fuoni .

"Ni kweli imetoka ajali hapa Fuoni Gari aina ya Harrier imegongana na Bodaboda, Gari ni ya yule bwana mdogo mchezaji wa Yanga Fei, lakini ni ajali ndogo tu hakuna aliyeumia"-Mkuu wa Kituo Cha Polisi Fuoni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo