Baba Aliyefanya mapenzi na Binti yake wa Kumzaa yamkuta makubwa

Mahakama ya Wilaya Mpanda, imemuhukumu Agustino Michese (59) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16.


Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Mpanda Rebeka Mwalusako amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti za mwezi wa tano hadi Disemba 30,2022 katika kijiji cha Isinde.

Amesema mtuhumiwa ametenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha (1) (a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2019.

Hatahivyo mtuhumiwa wakati akisomewa maelekezo ya awali alikili kutenda kosa hilo huku akijitetea alikuwa amelewa hivyo alijua anaefanyanae tendo hilo ni mke wake.

Upande wa mashitaka umeleta mashahidi watano akiwemo mtoto mwenyewe ambapo mtoto huyo ambae jina lake limehifadhiwa wakati akitoa ushahidi wake alisema baba yake amemfanyia kitendo hicho mara tatu huku akimtaka kutopiga kelele endapo atapiga atamfanyia kitu kibaya.

Ndipo alichukua maamuzi ya kumuelezea shangazi yake kutokana na kile anachofanyiwa na baba yake huku akidai hakuweza kumwambia mama yake kwababu ana matatizo ya akili hivyo alihofia alimwambia hatolifanyia kazi suala hilo.

Shahidi mwingine ambae ni daktari aliemfanyia vipimo mtoto huyo ameiambia mahakama kuwa uchunguzi wa kitabibu umebaini ni kweli mtoto huyo aliingiliwa.

Amesema mbali nakubainika kuingiliwa pia mtoto huyo ilibainika kuwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa ambapo baba yake baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika kuwa na magonjwa hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo