Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania Mjini New York, Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa (UN).
Balozi Katanga anachukua nafasi ya Prof. Kennedy Gaston ambaye uteuzi wake Umetenguliwa na anarudiahwa nyumbani.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Aidha, Rais Samia amemteua amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania, Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu akichukua nafasi ya Dkt. Moses Kusiluka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.