Mkuu wa mkoa wa Morogoro FATMA MWASA ameagiza kuondolewa kazini Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbigili wilayani Kilosa kwa tuhuma za kugeuza ofisi ya kijiji kuwa nyumba ya kulala wageni.
Licha ya tuhuma hizo
lakini pia Mtendaji huyo anadaiwa kuhamisha fedha za serikali kwenda akaunti
binafsi ya benki ya mwanamke wake huku akijua fika kufanya
hivyo nikinyume cha sheria .
Kufuatia kwa tuhuma
hizo kunamlazimu mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa kumfukuza kazi ili
viongozi wengine waliopewa dhamana kuachana na mambo ya wizi wa fedha za serikali.