Wakamatwa kwa Kuvujisha Video Inayomuonesha Rais Akijikojolea

Waandishi sita wa habari nchini Sudan Kusini wamekamatwa kwa kusambaza picha na video zinazomuonesha Rais Salva Kiir akijikojolea.


Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni mnamo Disemba 2022, Rais Kiir anaoneshwa akijiendea haja ndogo huku wimbo wa taifa ukipigwa kwenye hafla.


Kufuatia tukio hilo mashirika ya kutetea haki za vyombo vya habari yanasema kuwa wafanyakazi sita kutoka shirika la utangazaji la serikali walikamatwa wiki hii, BBC inaripoti. Hata hivyo, Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) linasema video hiyo haikuonyeshwa kwenye kituo hicho.


Kulingana na Patrick Oyet ambaye ni rais wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Sudan Kusini, aliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba waandishi hao wanashukiwa kufahamu namna video hiyo ilivujwa. Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei naye aliiambia Sauti ya Amerika kuwa watu wanapaswa kusubiri kujua sababu ya wanahabari hao kukamatwa.


Sudan Kusini nchi mpya zaidi barani Afrika - mnamo 2011. Lakini nchi hiyo imekumbwa na mizozo mingi tangu wakati huo, ikivumilia migogoro ya kikatili, machafuko ya kisiasa, majanga ya asili na njaa.


Chanzo: UGC 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo