Atorokwa na Mwanamke Wake aliyemsomesha, Amuachia Watoto

Baba wa watoto watano kutoka kaunti ya Migori amewaacha Wakenya katika mshangao baada ya kufichua kuwa alimlipia karo mkewe wa zamani, ambaye baadaye alimtelekeza na watoto wao.


Tolbert Josephat alikutana na mama watoto wake akiwa bado katika shule ya sekondari na hata kumlipia karo ya kuanzia kidato cha pili hadi kidato cha nne.


Baba huyo wa watoto watano mwenye umri wa miaka 33 aliambia TUKO.co.ke kwamba hakuishia hapo kwani pia alimlipia karo nzima ya chuoni hadi alipokuwa daktari.


"Imekuwa miaka mitatu tangu mimi na mke wangu tuachane na miaka sita ya kuwalea binti zangu watano peke yangu," Josephat, baba asiye na mke alisema.


"Nilimlipia mke wangu karo ya shule tangu alipokuwa kidato cha pili. Baadaye akawa daktari," aliongeza. Tolbert, mhandisi wa umeme kutoka kaunti ya Migori, alisema haikuwa nia yake kuishi maish ya useja, lakini ana furaha kulea binti zake peke yake.


Miaka miwili baada ya mke wake kuwa daktari, alimwambia Josephat kwamba hataki tena kuolewa, na walitengana kwa mwaka mmoja. “Kutoka hapo imekuwa ni mambo ya huku na kule, mwisho nikamwambia nimechoshwa na ndoa ya kuvutana ni heri tuachane,” alisema baba huyo wa watoto watano. “Hivyo ndivyo nilivyoishia kuachwa na upweke, sikumpokonya gari nililomnunulia kwa sababu nina magari mengine,” aliongeza Josephat.


Pamoja na kufurahia kulea mabinti zake peke yake, Josephat alisema changamoto pekee aliyonayo ni kwamba kuna wakati watoto wanatamani kuwa na mama yao.


Bado anachanganyikiwa na jinsi mke wake wa zamani alivyomtelekeza yeye na watoto wao na hajawahi kuwajulia hali hata mara moja. "Nimejifunza kuwa binadamu hana shukrani. Wewe fanya yako na uende. "Jifanyie kazi kwa bidii na jitahidi kupata pesa zako. Hata wazazi hawapaswi kutumaini kwamba watoto wao watawasaidia watakapokuwa wakubwa," aliambia TUKO.co.ke.

Chanzo:Tuko


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo