Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM, CDE Ali Mohamed Kawaida, amemuomba Rais na Amiri Jeshi mkuu Mh Dkt Samia Suluhu Hassan vijana wafupi nao wapate nafasi jeshini tofauti na ilivyo sasa. Kawaida amesema vijana warefu wanapewa zaidi kipaumbele zaidi ya wafupi katika jeshi la polisi.
Amesema hayo leo January 10, 2023 alipokuwa katika kilele cha matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Kauli hiyo imemuacha Mh Rais Dkt Samia kucheka pamoja na wageni waalikwa na wananchi kwa ujumla.
“Ombi la vijana wa Kitanzania kupitia kwenye Jeshi letu la Polisi, hatujui kama ni kanuni, utaratibu ama ni sheria yao ya kuwakataa vijana wenye asili ya ufupi na kuwaruhusu vijana wenye asili ya urefu. Huku ni kuonesha kutukataa vijana ambao tuna asili ya ufupi na kuwapata kipaumbele vijana wenye urefu wakisahau kwamba jukumu la ulinzi na usalama wa taifa hili ni la vijana wote tukiwemo sisi wafupi,” amesema Kawaida.
Kawaida amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana katika taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo ndani ya jeshi hilo.
Una maoni gani?