Halmashauri ya Wilaya Makete imeanza Ujenzi wa Jengo (Ghorofa moja) ambalo mpaka kukamilika kwake litagharimu Bilioni 3 ikiwa mpaka sasa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1 kuanza ujenzi
Akieleza kuhusu mradi huo Mtaalamu kutoka Divisheni ya Ujenzi Mhandisi White amesema Ujenzi huo unafanyika kupitia Chuo cha Sayansi na Teknolojia Must Mbeya kupitia kamouni yake ya MCB Company Limited
Kamati ya Siasa CCM Wilaya ya Makete imefika eneo linapojengwa jengo hilo (Ngiu) kwa lengo la kuangalia mwanzo wa ujenzi na kuhimiza umakini katika usimamizi
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Hawa Kader amesisitiza uwazi katika manunuzi ambayo yanafanywa na Halmashauri
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement Ngajilo amepongeza Viongozi wa Halmashauri kwa ubunifu katika kipindi kifupi huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi huo pamoja na viongozi wengine kuleta maendeleo katika Wilaya ya Makete
Diwani Kata ya Iwawa Mhe. Francis Chaula kwa niaba ya wananchi wa mji mdogo Iwawa ameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa katika Kata yake ikiwemo Ujenzi wa Hospitali ya wilaya na Jengo la Halmashauri.