Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema serikali imejipanga kuwashawishi vijana wanaotumia muda mwingi kucheza kamari (ku-bet), na badala yake wajikite katika shughuli za kilimo kwani inao mradi maalum utakaovutia vijana.
Katika mradi huo Serikali inatarajia kutoa mafunzo ya miezi mitatu kwa vijana Kutoka halmashauri mbalimbali nchini, kisha itawapa mashamba yaliyosafishwa pamoja na mbegu ili waanze kufanya kilimo cha kibiashara zaidi.