Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 5 Januari 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Rais Samia amemtumbua Kamishna Diwani, ikiwa zimepita siku mbili tangu amteua tarehe 3 Januari 2023. Awali, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
“Rais Samia ametengua uteuzi wa Kamishna Diwani, aliyemteua tarehe 3 Januari 2023. Aidha, Rais Samia amemteua Mululi Majula Mahendeka, kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Mahendeka alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Ikulu,” imesema taarifa ya Zuhura.