Afisa wa polisi nchini Kenya aliyefunga ndoa Desemba mwaka jana, amefumaniwa chumbani akiwa na mke wa mtu, katika nyumba moja mtaa wa Eastlands jijini Nairobi.
Mwanamume huyo aliyemfumania Afisa wa Polisi, imeelezwa kwamba alikuwa amesafiri kwenda kijijini na aliporudi nyumbani akamkuta mkewe akimsaliti.
Baada ya majibizano ya muda mfupi, mwanamume ambaye amefahamika kwa jina la Ali Abdul Majid, alihisi kutishiwa maisha na kuamua kupiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Dondora.
Maafisa wenzake mtuhumiwa waliotoa michango katika sherehe yake ya harusi walishangazwa kabisa na kisa hicho.