Polisi wafukua kaburi la aliyefariki kisha kuonekana tena

Hatimaye Jeshi la Polisi Kigoma kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji cha Kandaga Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wamefukua kaburi la Mtu aliyedaiwa kufariki April 2022 na baadaye kupatikana akiwa hai mwezi December mwaka jana.


Zoezi hilo limefanyika mbele ya Wataalamu wa Afya ambao wamechukua sampuli baada yakukutwa kwa mwili huo ambazo zitapelekewa kwa Mkemi Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba.

Itakumbukwa April 19,2022 katika eneo la Mazungwe Wilayani Uvinza kulitokea tukio la gari kugonga Mtu ambapo Ndugu wa Henry James alifika katika Kituo cha Afya Kazuramimba na kudai kutambua mwili wa aliyefariki katika tukio hilo kuwa Ndugu yao kisha taratibu za mazishi zilifanyika baada ya kukabidhiwa mwili na Jeshi la Polisi.

January 02 mwaka huu Kamanda wa Polisi Kigoma, Filemon Makungu alisema Mtu huyo ambaye alibainika kuwa na matatizo ya akili atafanyiwa uchunguzi wa kisayansi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hai.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo