Kesi ya Nccr - Mageuzi ya Mbatia na ile ya Selasini, watu Wafurika Mahakamani





Mamia ya Wafuasi wa NCCR-Mageuzi wamefika katika viunga vya Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi namba 570 itakayo amua ni nani wadhamini halali wa chama hicho. 


Ikumbukwe upande wa kina Joseph Selasini kesi yao namba 413 yakuomba kutambulika kama wadhamini halali wa chama ilishatupiliwa mbali na mahakama kuu kutokana na kukosa mashiko ya kisheria na kukiuka vifungu vya kisheria ikiwa ni pamoja na kosa la kumshitaki Marehemu.


Hadi sasa kesi zilizofutwa kwa kukosa Mashiko ya kisheri za Kina Joseph Selesini ni mbili kesi no 459 na kesi no 408 zote zimetupiliwa mbali na Mahakama Kuu.


Joseph Selasini na wenzake waliiomba Mahakama kuu iwatambue kama wadhamini halali wa chama cha NCCR-Mageuzi kesi iliyofunguliwa na Beat Mpitabakana na wenzake lakini kesi hiyo namba 459 ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu kwa kushindwa kukidhi vigezo vya kisheria hivyo kukosa uhalali wa kuendelea kuwepo mahakamani.


Baada ya kesi hiyo kutupwa nje ya Mahakama Wadhamini halali wa Chama walifungua kesi ya sasa ya kuitaka Mahakama isikubaliane na uovu uliofanywa na Kikundi cha kina Joseph Selasin kuwaondoa wadhamini halali wachama kwa kikao kisicho halali na utaratibu usio halali kinyume na Katiba ya NCCR-Mageuzi. 


Kesi hii itasikilizwa leo kuanzia saa 5 Asubuhi mbele ya Jaji Kisanya, ikumbuke uamuzi wa shauri hili unaweza kuamua hatma na muelekeo sahihi wa NCCR-Mageuzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo