Mwanafunzi wa chuo aliyepotea akutwa amekufa kwa mpenzi wake

 

Mwanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, aliyetoweka wikendi iliyopita, alipatikana amefariki katika nyumba ya mpenzi wake mtaani Kahawa Wendani, Kaunti ya Kiambu.


Victoria Muthoni Theuri, mwanafunzi aliyesomea Sera ya Umma na Utawala, alionekana mara ya mwisho Siku ya Krismasi.

Siku hiyo, aliwaambia wazazi wake wanaoishi katika eneo jirani la Kahawa Sukari katika Kaunti ya Kiambu kwamba alikuwa akimtembelea dadake.

Jioni ya siku hiyo, wazazi wake walimpigia simu dada yake ili kujua kama angelala nyumbani kwake.

Kulingana na polisi, dadake alisema hakuwa amemuona.

Wazazi waliamua kumpigia simu, lakini simu yake ilikuwa imezimwa.

Alipokosa kurudi nyumbani siku iliyofuata huku simu yake ikiwa bado imezima, wazazi wake waliripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi cha Kahawa Sukari.

Imeibuka kuwa kwa muda, alikuwa akipitia nyumbani kwa mpenzi wake kabla ya kwenda nyumbani baada ya shule.

Mwili wake ulipatikana na wakazi waliolalamikia harufu kutoka kwa chumba kilichokuwa kimefungwa.

“Mwanamume anayeishi hapo hakuwepo na tuligundua kuwa kulikuwa na harufu mbaya kutoka kwa nyumba. Ilinuka kama kitu kilichooza ndani ya nyumba iliyofungwa,” jirani alisema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo