Hebu fikiria hili; ni siku kuu ya Krismasi, na unarejea nyumbani kutoka kazini, ila ukifika unamkuta mumewe akiwa na mpango wa kando kitandani mwako.
Kutonesha kidonda hata zaidi, anakupiga kwa kumkatizia asirushe roho na mpango wa kando. Hii sio sinema ya Tyler Perry ila ni mambo yalimkumba mwanamke wa Mathare Aida Nekesa. Kwa mujibu wa ripoti za Nairobi News, Nekesa anauguza majeraha baada ya mumewe Mganda Peter Wakube klumpiga mnamo Disemba 25, 2022, alipomfumania kitandani na mpango wa kando
Mwanamke huyo anayefanya kazi ya nyumba alirejea nyumbani kwake saa nane mchana, na kumkuta mumewe akirusha roho na kidosho mwingine. Kwenye ksei iliwasilishwa katika Mahakama ya Makadara, korti iliarifiwa kwamba Nekesa alibisha mlango alipowasili ila Wakube alikataa aingie. Alipofaulu kuingia, mumewe alianza kumpiga mateke na mangumi kwa kumkatizia kipindi chake cha mahaba.
Nekesa alijeruhiwa usoni na tumboni, na kuokolewana majirani waliomsindikiza hadi Kituo cha Polisi cha Mathare, kabla ya kumpeleka hospitalini. Mumewe Nekesa hatimaye alikamatwa na vipande vya picha ya mkewe aliyorarua kwa kuudhika, zilipatikana. Wakube alikiri mashtka yake na kuiomba mahakama imuonee huruma kwa sababu anajuta.
Chanzo: TUKO.co.ke