DC apiga marufuku wanaume kusimama na wanafunzi dakika 15

Serikali wilayani Ludewa imelazimika kupiga marufuku wanaume kusimama na mtoto wa kike anayesoma kwa zaidi ya dakika 15 katika mazingira yenye mashaka ,baada ya kufanya utafiti mwepesi na kisha kubaini kwamba kuna kundi kubwa la watoto wa kike wanaokatisha masomo kwa kupata mimba za utotoni.


Awali akizungumza katika kikao cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu mkoa kilichohudhuliwa na naibu waziri wa tamisemi Dr Festo Dugange, mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere amesema punde baada ya kufika katika wilaya hiyo alibaini kuna ufaulu unaosababishwa na changamoto nyingi ikiwemo ya mimba na uhaba wa walimu na kisha kuja na mpango wa elimu ya makambi na katazo la wanaume kusimama na wanafunzi katika mazingira yasiyo rafiki.

Wakati wilaya ya Ludewa ikiweka mkakati huo na kisha kuinua ufaulu kutoka asilimia 60 hadi 80 katika kipindi cha miaka mitatu ,Serikali ya mkoa wa Njombe kupitia kwa katibu tawala Judica Omary imesema tatizo la upungufu wa walimu na mdondoko wa wanafunzi limekuwa kubwa hatua ambayo inamsukuma mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka kuweka msimamo mpya wa kuhimiza walimu kufundisha masomo ya ziada,Kuanzisha maabara binafsi za shule pamoja na kubariki wazo la kuanzisha makambi ya elimu mkoani humo.

Kwa upande wake naibu waziri wa TAMISEMI Dr Festo Dugange na Suzan Nusu ambaye ni Kaimu mkurugenzi wa elimu msingi TAMISEMI wanasema serikali imeendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu ili kuinua taaluma nchiniikiwa ni pamoja kuajiri walimu wapya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo