Kesi namba 2,2022 ya madai ya fidia ya shilingi mil 100 iliyofunguliwa na msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe dhidi ya kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania KKKT mkoa wa Njombe aliyefariki dunia 2020 kwa ajari iliyohusisha gari aina ya Hiace yenye nambari za usajiri T298-DNE na Mercedez Benz Truck yenye no za usajiri T210-AHU mali ya kanisa imetajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa na kisha kupanga Februari 3, 2022 kuanza kusikiliza mashahidi wa kesi hiyo.
Kesi hiyo ambayo imekuja baada ya mlalamikaji kushinda trafic kesi no 6 ,2021 iliyotokea eneo la Kibena katika mlima Ichunilo Septemba 25,2020 ambayo ilimsababishia majeraha na kisha kupekelekea kifo cha Kaselida Karo Mlowe(29) baada ya kupambania uhai hospitalini ambaye hadi umauti unamkuta alikuwa na watoto wadogo watatu wanaomtegemea.
Katika kesi ya kwanza ya ajali ya barabarani iliyosimamiwa na hakimu wa wilaya ya Njombe Matrida Kayobo, Mahakama ilimkuta na hatia dereva aliyekuwa akiendesha gari la kanisa na yeye kukiri kosa na kisha kulipa faini ya sh.150,000 hatua iliyompa mamlaka mlalamikaji kuendelea na utaratibu mwingine wa kufungua kesi ya fidia dhidi ya mlalamikiwa.
Akizungumzia kesi hiyo Wakili wa upande wa mlalamikaji Gervas Semgamo kwa niaba ya mawikili wengine Emmanuel Chengula na Frank Ngafumika anasema baada ya hatua mbalimbali za keshiria juu ya shauri hilo kwa sasa wanaendelea kesi ya madai huku wakitegemea tarehe 3 ya mwezi wa pili kuanza kusikiliza kesi yao ya msingi.
“Leo imekuwa ni mara ya tatu kufika Mahakamani hapa kwa ajili ya kuandaa mambo mbali ili kwenda kwenye kesi ya msingi kwa hiyo zoezi limeenda vizuri na tunategemea tarehe iliyopangwa tutaanza rasmi kusikiliza kesi hii na imani yetu ni kwamba Mahakama itatenda haki”alisema Wakili Semgamo
TAZAMA VIDEO HIYO MWANZO MWISHO
Kesi hiyo inaendeshwa na hakimu Mfawidhi wa mkoa wa Njombe Liad Chamshama huku wakili wa upande wa mlalamikiwa ambaye ni kanisa la Kiinjili la Kilithuri Tanzania Dayosisi ya kusini akiwa ni Marco Kisakali.